Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara adaiwa kuuza kiwanja feki

Hukumu Pc Data Mfanyabiashara adaiwa kuuza kiwanja feki

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashahidi 9 na vielelezo vinne vinatarajia kutolewa katika kesi kujipatia fedha kiasi cha Sh105 milioni inamkabili mfanyabiashara Abubakar Hassan (66).

anakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo la kujipatia kiasi hicho cha fedha baada ya kuuza kiwanja kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro pamoja na kughushi nyaraka.

Wakili wa Serikali Grace Mwanga, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ya jinai namba 17/2023 ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali.

Wakili Mwanga amemsomea PH, mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ferdnadri Kiwonde.

Akimsoma maelezo hayo, Wakili Mwanga alidai kuwa Machi, 2014 mshitakiwa akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani walijitambulisha kwa mtu anayefahamika kama Rajesh Agarway kwamba wanauza kiwanja kilichopo moshi mjini.

Alidai kuwa Rajesh alikubali kununua eneo hilo baada ya mshitakiwa na mtu mwingine ambaye hayupo mahakamani kujitambulisha kwake kama mume na mke Ebenezer Mwasha.

Alidai kuwa Rajesh alikubali na kuingia mkataba wenye jina la Ebenezer Mwasha uliosainiwa Machi, 2014 na mshitakiwa pamoja na Rajesh Agarway.

Hata hivyo, mshitakiwa alipokea hundi ya malipo ya Sh100 milioni kama sehemu ya malipo na baadaye Rajesh alilipa Sh5 milioni.

Alidai kuwa wakati biashara hiyo inaendelea mshitakiwa akiwa eneo la Azikiwe katika jengo la Benjamini Mkapa aliwasilisha hati feki ya kiwanja, kadi ya kupigia kura iliyoghushiwa pia alisema yeye ni mume wa Joyce Sengwaji.

Mwanga alidai kuwa wakiwa eneo hilohilo Rajesh aligundua kama hati hizo ni feki na zimeghushiwa na kutoa taarifa katika kituo cha polisi na mshitakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani hapa Januari , mwaka huu 2023 kwaajili ya kuhojiwa.

Baada ya mshitakiwa kusomewa hoja hizo alikubali taarifa zake binafsi na kukataa mashitaka yanayomkabili.

Hakimu Kiwonde baada ya kusikiliza hoja hizo aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 6, 2023 kwa ajili ya kuanza usikilizwaji.

Mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Katika kesi ya msingi, Machi mosi, 2014 Mtaa wa Azikiwe Ilala, Dar es Salaam katika eneo la jengo la Benjamin Mkapa, lililopo Posta mpya, mshtakiwa akiwa na nia ovu alijipatia Sh 105 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Rajesh Agarway akijifanya kuwa anamuuzia kiwanja kilichopo Moshi mjini wakati akijua siyo kweli.

Katika shitaka la pili inadaiwa kuwa kati ya tarehe na mahali pasipojulikana mshitakiwa alighushi hati na kujipatia hati ya kiwanja kilichopo eneo la Moshi Mjini kuonesha kuwa hati hiyo imetolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati akijua sio kweli.

Shtaka la tatu inadaiwa kuwa kati ya eneo na tarehe isiyofahamika mshitakiwa alitengeneza kadi ya kupigia kura ikionyesha kuwa ni halili na imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yenye jina la Ebenezer Shilekiromuu Mwasha wakati akijua siyo kweli.

Katika shitaka nne inadaiwa kuwa Machi Mosi, mwaka 2014 mshitakiwa akiwa katika Mtaa wa Azikiwe eneo la Jengo la Benjamin Mkapa, Ilala Dar es Salaam kwa nia ovu alijifanya kuwa yeye ndio Ebenezer Shilekiromuu Mwasha kwa lengo la kujipatia fedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live