Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara achinjwa kama kuku Manyara

 Lucas Mwakatundu Mfanyabiashara achinjwa kama kuku Manyara

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na Mfugaji Mkazi wa kijiji cha Losinyai,wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara ,Thomas Salimu(30)ameuawa kinyama kwa kuchinjwa kama kuku na kutengenishwa na kiwiliwili na mtu anayedaiwa ni rafiki yake.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea kati ya saa 8 na saa 9 usiku wa kuamkia leo baada ya mwili wa marehemu kukutwa barabarani majira ya asubuhi na wapita njia waliotoa taarifa kwa ndugu na jamaa wa marehemu.

Mwenyekiti wa kijiji hicho ambaye pia ni kaka wa Marehemu, Kapiliti Salimu alisema marehemu mdogo wake aliuawa kwa kuchinjwa na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Lentony Saning'o.

Alisema kuwa marehemu kabla ya kifo chake ,walionekama kuwa na mtuhumiwa wakinywa pombe pamoja na ilipofika majira ya usiku mtuhumiwa alimwomba marehemu kumpeleka nyumbani kwake kwa kutumia usafiri wake wa pikipiki .

"Kabla ya tukio marehemu walikuwa pamoja na mtuhumiwa wakinywa pombe na ilipofika majira ya usiku mtuhumiwa alimwomba marehemu waondoke na ampeleke nyumbani kwa kuwa marehemu alikuwa na usafiri wa pikipiki lakini wakiwa njiani ndipo mtuhumiwa alipomkaba na kumchinjwa na kisha kumpora kiasi cha sh,milioni 1.8 na kuondoka pia na pikipiki yake "

Aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akituhumiwa kutenda makosa mbalimbali kijijini hapo ikiwepo ubakaji na inasemekana huenda akawa na matatizo ya akili.

Alisema mbali na tukio hilo la mauaji mtuhumiwa alimpora kiasi cha sh,milioni1.8 pamoja kuondoka na pikipiki ya marehemu hadi asubuhi alipokamatwa na wananchi akiwa na pikipiki hiyo na kufikishwa kituo cha polisi cha Olkesiment wilayani humo.

Mwenyekiti hiyo alisema mwili wa marehemu wameuhifadhi katika mochwale ya kituo cha Afya Murieth jijini Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi na taratibu za mazishi.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayomkabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live