Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara Utalii adai kukamatwa na polisi, amuangukia Samia

Mfanyabiasha Samia Madai (600 X 428) Mfanyabiashara Utalii adai kukamatwa na polisi, amuangukia Samia

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara wa huduma za magari ya Kusafirisha Watalii Simon Njeri amedai Kukamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, huku lilishikilia Simu, Laptop, pamoja na Hati ya kusafiria kwa zaidi ya Juma moja na Nusu.

Njeri ambaye ni Mmiliki wa kampuni ya Utalii ya Utalii ya Impala Shattle kwa upande wa Kenya, akishirikiana na Mwenzake wa Tanzania anayefahamika kwa Jina la Edmund Robert Koka, amesema kadhia hiyo imempata wakati alipokutana na mwenzake ili wajadiliane namna ya kuwalipa madera wa kampuni hiyo ambao wana madai ya zaidi ya miaka miwili.

Ameiomba Serikali ya Tanzania Kupitia kwa Rais Samia Kuingilia kati, kwani anahisi Mwenzake anashirikiana na jeshi la Polisi ili kumgandamiza, kwa kuwa, alikamatwa wakiwa kwenye kikao, na amehojiwa na polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo la kuingilia mawasiliano.

Kwa upande wake mfanyabaishara KOKA amesema jambo hilo lipo polisi kwa Uchunguzi zaidi na Hawezi kutolea ufafanuzi licha ya Kumfahamu Mmiliki mwenza wa Impala Shattle.

Hata hivyo jeshi la Polisi Mkoani Arusha kupita kwa Kamanda Wake Justine Masejo amesema hana Taarifa za kukamatwa au kushikiliwa kwa Vifaa vya Mfanyabiashara Simoni Njeri, na anaendelea kufuatilia ili kujua ukweli wa Jambo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live