Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara Porojo akamatwa na gramu 300 za heroin

12074 PIC+POROJO TanzaniaWeb

Wed, 15 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imemkamata Ally Mohamed Yusufu  maarufu kama 'Porojo', akiwa na gramu 300 za dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni aina ya heroin.

Akizungumza na MCL Digital leo Agosti 15, 2018  Kamishna wa Intelijensia wa DCEA, Fredick Kibuta amesema Agosti 14 mwaka huu saa 8 usiku, Porojo alikamatwa akiwa na dawa hizo zilizofungwa kwenye mfuko wa plastiki.

Kibuta amesema maofisa wa mamlaka hiyo walifanya upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa huyo na kukuta unga huo ambao umepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini ni wa aina gani.

 

"Vipimo vya awali vilivyofanywa na wataalamu wa mamlaka hiyo vinaonyesha kuwa dawa hizo ni heroin hivyo upimaji kamili utafanywa na mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya hatua za kimahakama,"amesema Kibuta.

Kibuta amesema mamlaka hiyo inafahamu kupitia uchunguzi wake uliofanywa kwa muda mrefu inafahamika mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu kwa miaka mingi.

“Katika biashara zake ameshatembelea nchi mbalimbali ikiwamo Pakistani, Italia na Uturuki na mtandao wake upo ndani na nje ya nchi,” amesema.

Baadhi ya washirika wake katika biashara hiyo wamo wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya kama ambao baadhi yao walikamatwa mwaka huu na dawa za kulevya aina ya heroin na wote wameshafikishwa mahakamani.

Chanzo: mwananchi.co.tz