Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara Dar akamatwa na askari wa uhamiaji

9776 Mosha+pic TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Davis Mosha amekamatwa leo mchana Agosti 2, 2018 kwa madai ya akiwazuia askari wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza na MCL Digital msemaji wa idara hiyo, Ali Mtanda amesema Mosha amewashambulia askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori, jijini hapa.

"Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja,” amesema Mtanda.

“Wakati wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang'anya askari mmoja simu yake.”

Amesema alichofanya Mosha ni kinyume cha sheria ya uhamiaji namba 54 kifungu cha 45 kipengele 1 F, kinachozungumzia kumzuia ofisa wa uhamiaji kufanya kazi yake ya ukaguzi.

Akizungumza na MCL Digital, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema tayari  wamepokea taarifa ya tukio hilo, wanafanya uchunguzi kwa hatua za kisheria.

"Tunachunguza ili kujua kilichotokea ni nini, baada ya hapo ndio hatua nyingine zitafuata,” amesema Murilo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz