Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Mfalme Zumaridi' wenzake wafikishwa mahakamani

Zuma Pic Data 'Mfalme Zumaridi' wenzake wafikishwa mahakamani

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.

Msafara wa magari matatu aina ya difenda zilizolindwa na askari waliojihami kwa silaha umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema "Mimi ndiyo Mfalme Zumaridi" huku akionyesha ishara ya kuomba.

Miongoni mwa waliofanikishwa mahakamani hapo wakiwa na mhubiri huyo ni vijana wanaokadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 45 na wazee wa jinsia zote wanaodhaniwa kuwa na umri kuanzia miaka 45 hadi 65.

Watuhumiwa wako ndani ya mahakama wakisubiria hakimu wa kesi hiyo kuwasili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live