Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messina Denaro: Kiongozi wa 'Mafia' atiwa mbaroni

Matteo Messina Denaro Messina Denaro

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Mafia, Matteo Messina Denaro akamatwa mjini wa Sicily nchini Italia katika msako uliohusisha askari 100 wakati akiwa anafanyiwa matibabu katika hospitali mojawapo ya mji huo.

Matteo Denaro amekuwa akitafutwa kwa muda wa miaka 30 bila kubainika mahali alipo huku alikuwa anatoa amri zakiharifu akiwa mafichoni.

Inasemekana kuwa alibadilisha muonekano wa sura yake ili asikamatwe hivyo askari wametumia teknolojia kuweza kupata taswira ya sura yake ya sasa.

Pia, Matteo alishapewa hukumu nyingi za vifungo gerezani lakini hakuwahi kuhudhuria vifungo hivyo wala kufika jela.

Kikundi hicho cha Mafia kina julikana sana kwa vitengo vingi vya kiharifu kama usafirishaji wa madawa ya kulevya, mauwaji ya watu na majaji wawili mwaka 1993 waliokuwa wanapinga kikundi hicho na milipuko ya mabomu katika sehemu mbalimbali ya miji ya Italy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live