Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja kituo cha mafuta Kibaha jela miaka mitano

Meneja kituo cha mafuta Kibaha jela miaka mitano

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoa wa Pwani imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela meneja wa kituo cha mafuta cha Ukodi International Limited, Malima Charles baada ya kumkuta na hatia ya kuvunja ofisi na kuiba.

Akisoma hukumu hiyo leo Jumatatu Machi 9, 2020 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Joyce Mushi ameeleza kuridhishwa na ushahidi wa Serikali na kwamba adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wengine waliopewa jukumu la kusimamia vituo vya mafuta.

Amesema amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa makosa yote mawili.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, wakili Auleilia Mushi amesema mtuhumiwa alifanya njama za kuvunja ofisi na kuiba Sh45,266,133 za mwajiri wake wakati akijua kufanya hivyo ni kosa.

Amesema alifanya kitendo hicho Desemba 24, 2018 na kuchukua kiasi hicho cha fedha zilizokuwa za mauzo ya siku hiyo.

Charles maarufu Mukama alipopewa nafasi ya kujitetea ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na ana familia inamtegemea, ombi ambalo halikukubaliwa.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz