Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Membe agoma kumsamehe Musiba "Mali zake zitapigwa mnada"

Musiba Membe 01 Membe na Musiba

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bernard Kamilius Membe, waziri waziri wa zamani wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, amegoma kumsamehe mdai wake – Cyprian Musiba – aliyeamriwa na Mahakama Kuu, kulipa fidia ya takribani Sh. 9. 9 bilioni, kama fidia kwa kuchafua jina lake.

Katika barua yake kwa Askofu Emmanus Mwamakula, Membe amesema, “…Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri popote, na hata kama amesalimu, basi amechelewa.”

Anaongeza, “hata kama Musiba hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada.”

Membe alikuwa akijibu barua ya Askofu Mwamakula aliyemtaka mwanasiasa huyo, kumsamehe Musiba kwa maelezo kuwa hana fedha za kulipa fidia na hana uwezo wa kulipa kile alichoekelezwa na Mahakama Kuu.

Membe alikuwa amefungua shauri mahakamani kulalamikia Musiba – aliyejiita mwanaharakati huru – kuchafua jina lake; kumdhalilisha, kumzushia uwongo na kumkashifu.

Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kupitia hukumu yake iliyotolewa na Jaji Joacquine De Mello, Alhamisi ya 28 Oktoba 2021, ilijiridhisha kuwa Membe alivunjiwa heshima yake na hivyo, kuamuru Musiba kulipa Sh. 6 bilioni, pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi.

Aidha, Mahakama imemzuia Musiba, kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.

Akijibu kwa makini barua ya Askofu huyo Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho nchini, Membe alisema yafuatayo:

“Asante kwa barua yako ambayo umenitaka nimsamehe Musiba kwa sababu amesalimu amri na kwamba hana hela ya kunilipa hata kama atauza kijiji.

“Baba Askofu, sababu ulizozitoa hazina mashiko kwa sababu Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri popote, na hata kama amesalimu, basi amechelewa!

“Hata kama hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada.

“Musiba anajua kuwa siwezi kumsamehe kwa sababu nilimpatia nafasi tatu za wazi za kuomba radhi kwenye Chama akapuuza. Nilimpatia nafasi ya kuomba radhi kwenye magazeti yake akapuuza.

“Na kabla ya kesi haijaanza nilimpatia muda wa kulimaliza jambo hili nje ya mahakama, lakini nafasi zote hizo alizikataa.

“Kwa hiyo, Sitamsamehe kamwe na anastahili adhabu hiyo ili awe na adabu na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kijinga kama hizo.

Nawashukuru Majaji wote wa mahakama kuu kwa uvumilivu na kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kunirudishia heshima yangu na kuuthibitishia umma kuwa katika nchi hii kuna uhuru wa Mahakama na uongozi unaoheshimu sheria. Vinginevyo nakushukuru kwa barua na mawazo yako! Ubarikiwe!”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live