Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mdee na wenzake waliofukuzwa CHADEMA waanza kuhojiwa mahakamani

Tendega Waliofukuzwa CHADEMA waanza kuhojiwa mahakamani

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana Oktoba 7, 2022 Mawakili wa upande wa CHADEMA wakiongozwa na Peter Kibatala wameanza kuwahoji wabunge wa viti Maalum wanaopinga kufukuzwa uanachama wao na CHADEMA, ambapo Grace Tendega amekuwa mbunge wa kwanza kuanza kuhojiwa kuhusu namna walivyoupata ubunge wao.

Shauri hilo linalokuja kwa ajili ya kusikilizwa, ambapo ilianza kwa Mbunge wa Viti maalum Grace Victor Tendega kuhojiwa na jopo la mawakili wa upande wa wajibu maombi likiongozwa na Peter Kibatala ambaye alianza kwa kumhoji kuhusu nakala za viapo walizosaini yeye na wabunge wenzake wa viti maalum, waliofukuzwa Uanachama na CHADEMA, viapo ambavyo waliviwasilisha mahakamani.

Haya yanajiri katika kesi namba 36/2022 inayosikilizwa mbele ya Jaji Cyprian Mheka iliyofunguliwa na wabunge hao dhidi ya Chama cha Demokrasia Maendeleo CHADEMA, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya taifa ya uchaguzi.

Wakati Tendega akiendelea kuhojiwa wakawasilisha kielelezo namba moja ambacho ni moja kati ya vielelezo nane vilivyowasilishwa na uapande wa waleta maombi, ambayo ni flash yenye hotuba ya Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika alipozungumza na waandishi wa habari mnamo Novemba 25, 2021 baada ya wabunge hao kuapishwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13 ambapo waleta maombi wataendelea kuhojiwa na mawakili wao, ili kufafanua baadhi ya mambo aliyoeleza Tendega wakati akihojiwa na mawakili wa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live