Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji, wake zake wawili wapandishwa kortini Dar

74137 Mchungaji+pic

Tue, 3 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) na wake zake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kujibu mashtaka mawili, likiwemo la kuendesha shughuli za kidini bila kuwa na kibali.

Mbali na Chirhuza, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 175/2019 ni Esther Sebuyange (27) na Kendewa Ruth (26) ambao ni wake wa mchungaji huyo.

Mwingine ni Samwel Samy (22) ambaye ni mdogo wa Mchungaji huyo, wote wakiwa ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Jumanne Septemba 3, 2019 na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Augustina Mmbando.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Godfley Ngwijo na Sitta Shija, amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kuishi nchini bila kibali pamoja na kuendesha shughuli za kidini bila kuwa na kibali.

Katika shtaka la kwanza linalowakabili washtakiwa wote, inadaiwa, Septemba 2, 2019 huko Salasala, eneo la  Kilimahewa, wilayani Kinondoni,  Mchungaji, wake zake pamoja na mdogo wake walibainika kuwa wanaishi nchini  bila kuwa na kibali.

Pia Soma

Advertisement   ?
Katika shitaka la pili linalomkabili mchungaji pekee, inadaiwa siku na eneo hilo, Chirhuza alibainika  kujihusisha na kazi za kanisa akiwa hana kibali cha kuishi nchini.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, walikiri kutenda makosa hayo.

Mchungaji Chirhuza alikiri kufanya kazi ya uchungaji bila kuwa na  kibali.

Hakimu Mmbando ametoa masharti ya dhamana ambayo kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria au wawe watumishi wa Serikali.

Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo  hadi Septemba 9, 2019 ambapo upande wa mashtaka watawasomea hoja za awali( PH).

Hata hivyo, washtakiwa wote walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mchungaji huyo anadaiwa kuwa na wake watatu na  watoto sita ambapo  hata hivyo, mmoja hakufikishwa mahakamani.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz