Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji mbaroni tuhuma za kumbaka mwanafunzi makaburini

3e415ab4199b469601d3fc6b49de657b Mchungaji mbaroni tuhuma za kumbaka mwanafunzi makaburini

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mzee mmoja wa miaka 72 ambaye ni mchungaji wa moja ya makanisa yaliyopo wilayani Mbinga kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Simon Marwa Maigwa amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia mzee huyo ambaye alikamatwa mnamo Desemba 1, 2020 katika eneo la makaburini akiwa katika harakati za kumuingilia mtoto huyo kimwili.

"Wasamaria wema waliokuwa wakipita eneo hilo la makaburini walimuona mchungaji huyo akiwa amepiga magoti akimlazimisha mtoto huyo kufanya kitendo hicho na baada ya mhanga kuhojiwa alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchungaji huyo tangu 2019," amesema Kamanda Maigwa.

Chanzo: habarileo.co.tz