Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi akimfanyia maombi

Jela Miaka 30 Mchungaji mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi akimfanyia maombi

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Siloam lililopo katika Kijiji cha Manda Chini wilayani Rombo, Amani Upendo kwa madai ya kumbaka mwanafunzi wakati akimfanyia maombi.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema tukio hilo lilitokea Agosti 30, 2022 wakati binti huyo alipokwenda kwenye maombi, baada ya familia yake kuzunguka kwa muda mrefu kumtafutia tiba ya ugonjwa wa kuanguka uliokuwa ukimsumbua.

“Huyu mchungaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumbaka mwanafunzi, aliyekuwa na ugonjwa wa kuanguka, baada ya familia kujaribu kumtibu hospitalini pamoja na sehemu nyingine ikashindikana.

“Hivyo wakaamua kumpeleka kwenye maombi, kwa hiyo akiwa kwenye maombi ndipo mchungaji alipofanikiwa kumbaka," amesema Kanali Maiga.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, Mwenyekiti wa Kijiji Manda Chini, Ernest Mrosso amesema siku hiyo wakati tukio linatokea binti huyo alikuwa ametumwa kusaga mahindi aliporudi nyumbani alijiandaa kwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo kwa ajili ya kwenda kuombewa.

"Alipofika nyumbani aliacha ule unga akawa amekwenda kwenye maombi na alikuwa na wenzake ikafika mahali mchungaji akawaambia wale aliokuwa nao waondoke yeye ataendelea kumwombea binti huyo.

"Wakati akimwombea huyu mtoto alidondoka chini ndipo mchungaji alipomchukua na kwenda kumfanyia unyama huo aliofanya, hatimaye mtoto alipokuja kuzinduka ndio akakuta tayari amefanyiwa unyama huo ndipo alipochukuliwa na kupelekwa hospitali," amesema Mrosso.

Mwenyekiti huyo amelaani kitendo hicho huku akisema ni unyama ambao haufai kabisa kwa kiongozi wa kiimani kufanya tukio la namna hiyo na kusema ni kitendo ambacho kimeichukiza jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live