Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji aua Mchumba, amzika chumbani

Fekala Mchungaji aua Mchumba, amzika chumbani

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joseph Fekala; ni mchungaji kutoka eneo la Bayelsa nchini Nigeria ambaye anadaiwa kumuua mchumba’ke kwa deni la pesa za Nigeria, Naira elfu 50 (sawa na takriban shilingi 280,135 za Tanzania) kisha kumzika chumbani kwake.

Maofisa wa Polisi katika Jimbo la Bayelsa wamemkamata mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa madai ya kumuua Kate Ogwoh mwenye umri wa miaka 26.

Fekala ambaye ni mchungaji wa vijana katika kanisa la kipentekoste huko Yenagoa, alidaiwa kumnyonga Kate hadi kufa kisha kumzika kwenye kaburi lililopo chumbani kwake.

Inaelezwa kuwa kisa hicho kilitokea katika Kitongoji cha Okaka huko Yenagoa Julai 29, 2022.

Ripoti kadhaa ikiwemo ya The Nation zinasema kuwa mshukiwa alidaiwa kumuua Kate kutokana na deni la Naira 50,000 alilokuwa akidaiwa kutokana na nguo alizouziwa.

“Kate alikuwa akiuza nguo, mtuhumiwa alikuwa anadaiwa N50,000 na Kate alikwenda kuchukua pesa zake nyumbani kwake na hakuna aliyemuona hadi mwili wake ulipogundulika umezikwa chumbani kwa mtuhumiwa,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Ilielezwa kuwa hakuna aliyemsikia mama yake alipokwenda kumtafuta nyumbani kwa mwanaume huyo na kuliona kaburi hilo likiwa na kina kirefu, ndipo alipotoa taarifa.

Hadi kifo chake, alikuwa mshiriki wa Kanisa la Christ Embassy huko Yenagoa huku Joseph akiwa mchungaji wa vijana katika kanisa la kipentekoste.

Msemaji wa Polisi wa Bayelsa, SP Asinim Butswat alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa mshukiwa alikamatwa kufuatia taarifa hiyo kutoka kwa majirani mnamo Julai 29, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live