Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Nurdin mahakamani kwa kumbaka mtoto wake

Mchungaji Web Mchungaji Nurdin mahakamani kwa kumbaka mtoto wake

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Mchungaji wa kanisa la kilokole Nurdin Abdallah, amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa kosa la kumbaka kwa nyakati tofauti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita.

Ni Kesi namba 79 ya mwaka 2022, iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Erick Kimaro, katika Mahakama ya wilaya ya Magu inamkabili Mchungaji huyo anayedaiwa kumbaka binti yake wa kumzaa baada ya kumchukua kutoka kwa mama yake waliyeachana.

Inadaiwa kuwa mchungaji huyo aliachana na mke wake mwezi wa saba mwaka huu na mwanamke huyo akaondoka na kwenda kuishi wilayani Bunda mkoani Mara ndipo mchungaji akaamua kuishi na binti yake ambae inadaiwa amekuwa akimuingilia kimwili mara kwa mara hadi majirani walipogundua jambo hilo na kuamua kumuhoji mtoto huyo na kuwathibitishia kuingiliwa kimwili na baba yake huyo.

Aidha baada ya majirani kugundua kwamba binti huyo amefanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji walimpeleka kituo cha polisi na kufungua kesi kisha wakapewa fomu namba tatu ya polisi na kumpeleka hospitali na baadae binti huyo alikabidhiwa kwa afisa ustawi wa jamii wakati kesi ikiendelea.

Na leo hii Oktoba 12, 2022, mshtakiwa huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la kilokole lililopo Kisesa amewakilishwa mahakamani na mdhamini wake Bernard Mashauri aliyedai kuwa mshtakiwa Nurdin Abdalah anaumwa sehemu zake za siri zimevimba na kupelekea kushindwa kutembea.

Chanzo: Eatv