Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Kanisa la KKKT mbaroni tuhuma za kulawiti mtoto miaka 8

Images (42.jpeg Mchungaji Kanisa la KKKT mbaroni tuhuma za kulawiti mtoto miaka 8

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: Malunde

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikiria Mchungaji wa Kanisa la KKKT -Makedonia ya Lubaga lililopo mjini Shinyanga ambayo ni Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 8.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kukamatwa kwa Mchungaji huyo Agosti 12,2022.

"Tunamshikilia mchungaji (jina limehifadhiwa) kwa ajili ya uchunguzi zaidi na uchunguzi ukikamilika tutamtafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili", amesema Kamanda Magomi.

Chanzo: Malunde