Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchina amuua mchina mwenzie DAR

Screenshot 2022 06 12 At 16.32.04 660x400.png Mchina amuua mchina mwenzie DAR

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamtafuta Mtuhumiwa Zheng Lingyao (42) Raia wa China Mkazi wa Dar es salaam kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26), Raia wa China, Mfanyabishara na mkazi wa Kalenga Ilala Dar es salaam.

“Tukio hilo limetokea tarehe 11/06/2022 mtaa wa Kalenga Ilala kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa tano na dakika arobaini na tano usiku ambapo Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqin (32) Raia wa China na badaye alimfyatulia risasi FU, Raia wa China ambaye alipoteza maisha”

“Nie anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili, uchunguI wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi” Muliro Jumanne, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam

Chanzo: www.tanzaniaweb.live