Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchina amuua Mnigeria kwa kugoma kuolewa naye

Buhar Gang Mchina amuua Mnigeria kwa kugoma kuolewa naye

Mon, 19 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi huko Kano State, Kaskazini Maghrabi mwa Nigeria, limemkamata Mchina mmoja aliyefahamika kwa jina la Geng Quanrong, kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake wa muda mrefu, Ummukulsum Buhari, 23.

Tukio hilo limetokea Ijumaa iliyopita usiku katike eneo la Kabuga, Gwale huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi ambapo awali walikubaliana kuoana lakini baadaye mrembo huyo alimkacha Mchina na kuamua kuolewa na Mnigeria mwenzake.

Inadaiwa kuwa, hata baada ya mfarakano huo, Ummukulsum alihamia kwa bwana mpya, lakini baadaye walitibuana na akarejea nyumbani kwao kuendelea na maisha ya kawaida, baadaye uchumba na Mchinia uliendelea huku mwanaume akidai kuwa mpenzi wake huyo amemlia pesa zake nyingi na kumwaminisha kuwa atamuoa.

Msemaji wa jeshi la Polisi Kano, Abdullahi Kiyawa, amesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 47, alimsurubisha binti huyo kwenye fensi ya nyumba yake kwa muda mrefu ambapo mama wa marehemu alimsihi amwache lakini kipigo kiliendelea, ndipo mama huyo akalazimika kuita polisi haraka.

Baada ya polisi kufika walijaribu kumkimbiza hospitali haraka kwa ajili ya matibabu ili kuokoa uhai wake, lakini walipofika tayari alikuwa amepoteza maisha. Jeshi la Polisi limeihamishia kesi hiyo makao makuu ya jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Binti huyo ni mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kilimo katika Chuo Kikuu cha kampala nchini Uganda na kwa sasa alikuwa na mwaka mmoja akifanya kazi katika kituo cha National Youth Service Corps (NYSC) huko Sokoto State.

Siku chache zilizopita mrembo huyo na mpenzi wake walijirekodi video wakiimba wimbo wa ‘Nakupenda’ wa msanii Jay Melody kutoka Tanzania ambapo walionekana ni wenye furaha na wakifurahia mapenzi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live