Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Uhuru Selamani Atuhumiwa kwa Ubakaji

Uhuru Selamani 22 Mchezaji Uhuru Selamani Atuhumiwa Kubaka

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili mchezaji wa zamani, Uhuru Selemani Mwambugu umeielezea Mahakama ya Wilaya ya Temeke jinsi alivyombaka mtoto wa kike ambaye ni ndugu yake.

Wakili wa Serikali Gace Lwila akimsomea maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mfawidhi, Aziza Mbadjo alidai Aprili 13, 2021 maeneo ya Chang'ombe Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam mtoto huyo akiwa nyumbani kwao alitembelewa na ndugu yake ambaye mshtakiwa Mwambugu

Lwila alidai kuwa mshtakiwa huyo baada ya kufika nyumbani kwa mtoto huyo akamuuliza yupo na nani ndipo akamjibu yupo peke yake.

Alidai wakati huo mtoto huyo alikiwa amevaa kanga ndipo akamkaribisha ndani alipoingia alimlazimisha kwa nguvu na kuanza kumbaka.

"Alipomaliza kumfanyia kitendo hicho alimwambia asimweleze mtu yeyote akisema atamfanyia kitu kibaya," alidai Lwila.

Lwila alidai baada ya kufanyiwa kitendo hicho alimwambia dada yake ndipo wakaenda kituo cha polisi cha Chang'ombe kutoa taarifa ambapo walipewa fomu ya matibabu(PF3).

Alidai baadaye walienda hospitali na majibu ya daktari yalipotoka ikabainika ameingiliwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mbadjo aliahirisha shauri hilo had Machi 28, 2022 kwa ajili ya ushahidi.

Katika kesi ya msingi April 13, 2021 maeneo ya maeneo ya Chang'ombe Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam alimbaka mtoto wa kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live