Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kwenda kuondoa utendaji wa mazoea ili kuweka misingi ambayo itaifanya Tanzania kuwa namba moja Afrika na dunia katika sekta ya utalii.
Aidha Waziri Mchengerwa ameitaka TANAPA chini ya Mwenykiti wake wa Bodi Jenerali Mstaafu George Waitara kupambana na Vitendo vya ujangili ambavyo vimenza kurejea katika hifadhi mbalimbali nchini.
Waziri Mchengerwa ametoa kauli hii jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Waziri Mchengerwa ameitaka TTB iliyo chini ya Mwenykiti wao Balozi Dkt Ramadhan Dau kwenda kutatua mara moja changamoto zilizopo na kusimamia mikakati ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo amefafanua kuwa idadi ya vivutio vilivyopo nchini hailingani na mapato yanayopatikana.