Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge anayedaiwa kuua: Hata Mimi nataka kujua kilichomuua Olunga

Mbunge Wa Kenya Mbunge anayedaiwa kuua: Hata Mimi nataka kujua kilichomuua Olunga

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mbunge mteule wa Kimilili, Didmus Barasa kujisalimisha mapema leo Ijumaa, Agosti 12, 2022 kufuatia amri ya kitengo cha upelelezi wa jinai, mbunge huyo amekana tuhuma zinazomkabili za mauaji ya dereva wa mpinzani wake ambaye anatuhumiwa kumuua papo hapo kwa kumpiga risasi kichwani usiku wa Jumanne, Agosti 9, 2022 katika kituo cha kupigia kura.

Akikana tuhuma hizo, Barasa amedai kwamba na yeye pia anashangazwa na tukio hilo na anataka kujua nani alimuua dereva Brian Olunga ambaye alikuwa dereva wa mshindani wake mkuu katika kinyang’anyiro cha Kimilili, Brian Khaemba kutoka Chama cha DAP-K.

Akizungumza na vyombo vya habari punde baada ya taarifa kusambaa kwamba amejisalimisha kwa vyombo vya dola, mbunge huyo alisema anashirikiana na polisi wakati wanachunguza suala hilo na kusema kwamba hakuwa amekimbilia nchi Jirani ya Uganda kama ambavyo taarifa zilisambazwa zilisema.

“Nilikwenda Nairobi nikisubiri kukamatwa lakini nilipoona kwenye runinga kamanda wa polisi wa mkoa akinitaka nijisalimishe, niliendesha gari hadi eneo hili na niko tayari kutoa ushirikiano kwa polisi ili pia nijue nini kilimuua kijana huyo,” Barasa alisema.

Mbunge huyo alidai kuwa siku ya Jumapili, mmoja wa walinzi wake alivamiwa na kujeruhiwa vibaya na kwa sasa yuko hospitalini akiendelea na matibabu. Barasa alisema pia alishambuliwa siku hiyo hiyo na kuripoti kisa hicho kwa polisi.

“Kulikuwa na watu wengine waliokuwa na bunduki akiwemo mshindani wangu, afisa wa polisi aliyekuwa anasimamia vituo vya kupigia kura. Pia, tutakuwa tukitoa maombi kwamba silaha zote zilizokuwepo zifanyiwe uchunguzi wa kitaalamu,” alisema.

Mbunge huyo alijisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Bungoma na kuwekwa chini ya ulinzi huku uchunguzi wa kesi ya mauaji ukiendelea.

Siku ya Alhamisi, polisi walimpa muda wa saa sita awe amejisalimisha kwenye kituo chochote cha polisi, siku moja tu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP Noordin Haji kutoa kibali cha kukamatwa kwake baada ya kusemekana kuwa amekimbilia mafichoni baada ya kitendo hicho cha mauaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live