Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ahukumiwa jela miaka 67

Mbunge Ahukumiwa Jela Miaka 67.png Mbunge ahukumiwa jela miaka 67

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: Radio Jambo

Mahakama kuu imeidhinisha kifungo cha miaka 67 cha Mbunge wa Sirisia John Waluke kuhusiana na kesi ya bodi ya nafaka na mazao (NCPB) inayohusisha Shilingi milioni 313.

Jaji Esther Maina alisema mashtaka dhidi ya Waluke na Grace Wakhungu yaliyokuwa mbele ya Hakimu Elizabeth Juma yalithibitishwa bila shaka yoyote.

"Adhabu hazikuwa kubwa zaidi. Zipo ndani ya sheria. Hatia na hukumu zimethibitishwa," alisema Jaji.

Maina alisema Waluke na Wakhungu watalazimika kulipa faini au kutumikia vifungo hivyo.

Wakhungu kwa upande wake alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 69 gerezani. Iwapo hawatalipa faini zilizowekwa na mahakama ya mwanzo ambayo ni zaidi ya shilingi Bilioni mbili, watalazimika kutumikia kifungo cha muda mrefu gerezani.

Wawili hao waliachiliwa kwa dhamana ya Shilingi 10 milioni na milioni 20 mtawalia mnamo Septemba 2020 baada ya kukaa jela kwa miezi mitatu.

Walifungwa Juni 22, 2020 na Mahakama ya Kupambana na Ufisadi baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai na kujipatia Sh297 milioni kinyume cha sheria kupitia mikataba ya ukora katika Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB).

Wawili hao wanaweza kukata rufaa katika mahakama ya rufaa.

Chanzo: Radio Jambo