Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge aendelea kusota rumande

Kishapu Mbunge aendelea kusota rumande

Tue, 12 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MBUNGE wa Kishapu Suleiman Nchambi (CCM), amerudishwa rumande baada ya kesi yake inayomkabili ya tuhuma za uhujumu uchumi kuahirishwa kusikilizwa hadi Mei 25, mwaka huu.

Sababu za kuahirishwa ni Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi pamoja na utoaji dhamana.

Kesi hiyo ipo chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ushindi Swalo, ambapo kwa mara ya kwanza ilisomwa Mei 8, mwaka huu, na kutajwa kusikilizwa tena jana, na mtuhumiwa kurudishwa rumande.

Mbunge huyo ana shitakiwa kwa makosa 12 ya uhujumu uchumi na kufunguliwa kesi namba 10, 2020, lakini mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi wala utoaji wa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live