Dar es Salaam. Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara 'Bwege' anashikiliwa na polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai akizungumza na MCL Digital leo usiku Oktoba 1, 2018 amesema Bwege amekamatwa saa 10 jioni eneo la Maalim Seif lililopo Kilwa Kivinje.
Ngubiagi amesema mbali na Bwege wengine wanaoshikiliwa na polisi ni madiwani wanne akiwemo diwani wa Kilwa Masoko na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka.
"Bungara alipeleka barua ila kwa sababu za kiusalama polisi walizuia mkutano huo na yeye aliomba asiufanye. Endapo angefanya kungekuwa na uvunjifu wa amani," amesema Ngubiagai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo.