Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe mbaroni tuhuma kutakatisha mabilioni

545e5a106bca3536d765aaf37b22222c Mbowe mbaroni tuhuma kutakatisha mabilioni

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata ili kumuhoji mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya White Star Investment ya jijini Dar es Salaam Taalib Mbowe kwa tuhuma za kukwepa kodi na kutakatisha fedha haramu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Uhusiano wa Takukuru Doreen Kapwani, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni hiyo pia anatuhumiwa kwa kosa la udanganyifu.

Taarifa ya hiyo ilieleza kuwa, kampuni hiyo ya White Star Investment inashughulika na usafirishaji wa ndani na nje ya nchi kwa kutumia malori.

Kapwani alisema pamoja na uchunguzi huo, Takukuru pia inachunguza umiliki wa vichwa vya malori zaidi ya 100 yanayomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

Alisema pia anachunguzwa kutokana na mikopo yake ya zaidi ya dola za Marekani milioni tatu sawa na Sh bilioni 6.3 za kitanzania kutoka benki ya Barclays na Dola za Marekani 540,000 sawa na Sh bilioni 1.1 za kitanzania kutoka benki ya Equity.

“Uchunguzi huu ukikamilika na kuthibitisha tuhuma hizi, mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani,”alisema Kapwani.

Chanzo: habarileo.co.tz