Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe amefikishwa Mahakama Kuu, hatma ya kesi yake inasubiriwa leo

MBOWE12 Mbowe amefikishwa Mahakama Kuu, hatma ya kesi yake inasubiriwa leo

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi dhidi ya pingamizi walilowasilisha mahakamani hapo la kupinga kesi yao kusikilizwa na mahakama hiyo .

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Septemba Mosi, 2021 majira ya saa mbili asubuhi na kupelekwa mahabusu iliyopo mahakamani hapo.

Hata hivyo ilipofika saa 2:45 asubuhi, walitolewa mahabusu na kupelekwa ndani ya ukumbi wa mahakama, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa Jaji Luvanda.

Jana Agosti 31, 2021 Mbowe na wenzake waliwasilisha pingamizi mahakamani hapo wakipinga mahakama hiyo kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni divisheni maalumu.

Baada ya washtakiwa hao kuwasilisha pingamizi hilo, Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 3 ya Mwaka 2016 Makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo Mahakama ya Ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Kutokana na hoja hizo, Luvanda anayesikiliza shauri hilo, alipanga kutoa uamuzi leo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz