Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe afikishwa Mahakama ya Ufisadi

Video Archive
Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi Uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman mbowe inasomwa leo Agosti 31, 2021 hapa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi jijini Dar es Salaa kwa mara ya kwanza baada ya taratibu za kisheria kukamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbowe ameshafikishwa katika Mahakama hiyo, akitokea katika Gereza la Ukonga, huku jopo la Mawakili wake wakiwa tayari kwa utetezi, wafuasi wa Chama hicho nao hawako nyuma katika kufuatilia hatma ya kesi hiyo.

Mwenyekiti huyo alishtakiwa kwa makosa ya Uhujumu uchumi pamoja na ugaidi, na alikatamatwa Juni 20, mwaka huu 2021 akiwa jijini Mwanza kwenye kongamano la Katiba lililoendeshwa na idara ya vijana ya chama hicho BAVICHA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live