Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni wakitafuta soko la meno ya tembo

Pembe Moro Kamanda Musilimu baada ya kukamata watuhumiwa

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Morogoro inawashikilia watu wawili kwa tuhuma ya kukutwa na vipande 14 vya meno ya Tembo yenye uzito wa kilo 30.52 vikiwa vimehifadhiwa kwenye mabegi mawili madogo wakiwa katika harakati za kutafuta soko .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema Mei 6, 2022 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Jeshi hilo kwa kufanya misako, doria na oparesheni ili kukabili uhalifu na wahalifu.

Musilimu amesema watuhumiwa hao walikamatwa Mei 2, mwaka huu, majira ya saa nane mchana eneo la Nane Nane , Kata ya Tungi , Manispaa ya Morogoro kutokana na doria ya pamoja kati ya Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

Kamanda Musilimu amewataja watuhumiwa hao ni Shilla Simon (37), fundi ujenzi na mkazi wa wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya na wenzake Selemani Halphani (30) ambaye ni dereva wa Pikipiki (Bodaboda) ,mkazi wa Chimala, mkoani Mbeya .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live