Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni madai ya kumkaba mke na kumuua

Mtuhumiwa.webp Mbaroni madai ya kumkaba mke na kumuua

Thu, 14 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 55 (jina limehifadhiwa) mkazi wa Tarafa ya Kilyamatundu, wilayani Sumbawanga kwa tuhuma za kumkaba hadi kumuua mke wake Namsonga Bonifas (53), kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Justine Masejo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 9, majira ya saa mbili asubuhi wakati wanandoa hao wakiwa nyumbani kwao.

Alisema kabla ya tukio hilo wanandoa hao walirudi nyumbani usiku wakiwa wametoka kilabuni kunywa pombe na kisha wakaingia ndani ya nyumba yao kulala.

Asubuhi ya siku iliyofuata mmoja wa majirani hao alifika kwa lengo la kuwasalimia na kutaka kujua nini kilichotokea katika nyumba hiyo baada ya usiku kusikia wanandoa hao wakizungumza kwa kujibizana maneno makali.

Alisema alipofika na kugonga hodi mtuhumiwa huyo aliitika, lakini hakutoka nje hali iliyomlazimu jirani huyo kusukuma mlango na kuingia ndani na kukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala sakafuni akiwa amekwisha fariki dunia.

Alitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji na baadaye polisi ambao walipofika na kumkamata mtuhumiwa huyo.

Kamanda Masejo alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na watamfikisha kituo cha polisi baada ya upelelezi wa awali kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live