Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake

Mbaroni Mbaroni kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa Kijiji cha Luwayo, Wilaya Buikwe nchini Uganda, wamebaki na mshangao mkubwa baada ya mwanaume kudaiwa kumkatakata mpenzi wake hadi kufa.

Msemaji wa mkoa wa kipolisi wa Ssezibwa Hellen Butoto amesema uchunguzi kuhusiana na tukio hilo umeanza ilia kubaini chanzo cha mauaji ya Priscilla Agasiru yanayodaiwa kufanywa na baba wa mtoto wake.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, Ekurius Wazemba na babake, ambao ni wakazi wa eneo hilo, wamekamatwa kwa madai ya kuhusishwa na mauaji hayo ambayo yametokea Julai 11 katika kijiji cha Luwayo.

“Suala hilo liliripotiwa na kaka wa marehemu kuwa mwili wa dada yake ulichinjwa na kutupwa kando ya barabara ya kijiji cha Luwayo na mpenzi wake ambaye alizaa naye mtoto." amesema Butoto na kuongeza;

"Marehemu alikatwa maeneo mawili, kichwani na sehemu nyingine. Tuna washukiwa wawili chini ya ulinzi wa polisi ambao watatusaidia katika uchunguzi wetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live