Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa tuhuma za kuiba mtoto

10650 Mtoto+pic TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Polisi wanamshikilia mkazi wa kijiji cha Mbugani tarafa ya Buchosa wilayani Sengerema, kwa tuhuma za wizi wa mtoto wa kiume mwenye umri wa wiki tatu.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo Julai 3 kuwa mtuhumiwa ni mwanamke alikamatwa jana katika kijiji hicho na anadaiwa kutenda kosa hilo baada ya kukaa kwenye ndoa muda mrefu bila kupata mtoto.

Msangi amesema mwanamke huyo na mumewe anayejishughulisha na uvuvi visiwani maeneo ya Bukoba, wamekaa kwenye ndoa muda mrefu bila kupata mtoto.

Kitendo hicho kilimuumiza mwanamke na kuamua kumdanganya mumewe kuwa, amepata mimba na akaondoka eneo hilo kwenda kijiji cha Mbugani akidai amekwenda kulea mimba na kujifungua.

Amesema akiwa huko siku moja, alipita kwenye kijiji cha Bulyaheke akamuona mwanamke akinyonyesha mtoto mchanga kutumia fursa hiyo kumuiba.

“Juni 30, mtuhumiwa alimpigia simu mumewe na majirani zake kuwaambia kuwa anakwenda hospitali kujifungua, ilipofika saa mbili usiku alifika nyumbani kwa mwanamke aliyekuwa akinyonyesha mtoto kijiji cha Bulyaheke,” amesema Msangi na kuongeza:

“Alipofika, mama wa mtoto alikuwa nje anapika na yeye alipitia mlango wa nyuma na kwenda kumuiba.”

Baada ya kufanikiwa alianza kuwapigia simu majirani na mumewe kuwataarifu kuwa amejifungua salama, ingawa majirani walipata  shaka.

 “Hata hivyo, majirani walipata shaka na taarifa hizo kwa sababu tayari walishapata habari kuwa kuna mtoto ameibwa, walitoa taarifa polisi ambao walifanya uchunguzi wa haraka kisha mtuhumiwa kutiwa nguvuni,” amesema.

Amesema polisi walipofanya mahojiano naye alikiri kuiba mtoto, hivyo mtoto alirudishwa kwa mama yake na mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz