Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa mauaji ya mke wake

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe, Hamis Issah Mbaroni kwa mauaji ya mke wake

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia mkazi wa Kata ya Kihesa mkoani Iringa, Baraka Mtewe (30) kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mke wake Jackline Nyondo (27).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Oktoba 31, 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kabla ya kifo Jackline alikwenda Makambako kumsalimia mumewe lakini katika sintofahamu iliyotokea mumewe huyo alichukua kitu kizito na kumpiga nacho na hatimaye alipoteza maisha.

Kamanda Issah amesema baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alichukua mashuka na vitu vingine kisha kumfunika marehemu na baadae alifunga mlango na kutoweka pasipojulikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live