Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa madai ya kumuua mkewe

Mbaroni Kwa Madai Ya Kumuua Mkewe.jpeg Mbaroni kwa madai ya kumuua mkewe

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kutokana na utata wa kifo cha anayedaiwa kuwa mke wake Primrose Matsambire (39) raia wa Zimbabwe.

Primrose amefariki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi januari 11 alipopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kukutwa akiwa anatokwa na damu mdomoni akiwa nyumbani kwake Kiluvya Madukani Wilaya ya Kisarawe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo alieleza ,aliyegundua marehemu kutokwa damu kwa wingi mdomoni ni msichana wa kazi, baada ya kuona hali hiyo ya marehemu alienda kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kumpeleka katika hospitali ya Tumbi kwa matibabu.

Alisema mume wa marehemu hakuwepo wakati tukio hilo likitokea na kwamba anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na uchunguzi wa kina wa kifo cha mke wake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi huku chanzo cha kifo hicho kikiendelea kuchunguzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live