Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kuuza sukari bei kubwa

Pingu Law Mbaroni kwa kuuza sukari bei kubwa

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Sukari nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, imewakamata wafanyabiashara watano wa maduka ya jumla na rejareja baada ya kubainika kuwa wanauza kilo moja ya sukari kwa shilingi 4000 hadi 5000, tofauti na bei elekezi ya serikali ya shilingi 2,800 hadi 3,000.

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Afisa kutoka Bodi ya Sukari, ambaye ndiyo aliyeongoza oparesheni hiyo, George Gowele, amesema operesheni hiyo ililenga kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaoendelea kukiuka bei elekezi.

Aidha ameongeza kuwa licha ya serikali kufuta ushuru wa kuingiza sukari nchini lakini bado baadhi ya wafanyabishara wameendelea kukiuka bei elekezi iliyopangwa na serikali hivyo kuendelea kusababisha ugumu wa upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa walaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live