Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kutapeli vijana 76

Newslite Maigwa Kamanda Maigwa

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja ambaye jina limehifadhiwa kwa tuhuma za kuwakusanya vijana 76 kwa lengo la kuwapatia semina ya ujasiriamali jambo ambalo limebainika ni utapeli.

Mtuhumiwa huyo alikua akitumia majina ya viongozi akiwemo Wilium Lukuvi na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kwamba wanataarifa na anachokifanya hivyo atawapatia ajira baada ya mafunzo.

Kamanda Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, akisema alikuwa akijipatia Sh35,000 kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwalipia kila mmoja Sh300,000 kama ada baada ya kuhitimu mafunzo hayo na kwamba atawapatia ajira, hadi anakamatwa alikuwa ameshakusanya Shilingi milioni 2,100,000 kutoka kwa vijana hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live