Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Machia Mbasa (General) umri wa miaka 65 Mkazi wa Kijiji cha Lwafe Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga njama za kutaka kumuua Mabula Ntemange(37) baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo wakati yeye alipokuwa gerezani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na jeshi la Polisi kufuAtia kupata taarifa za kutaka kufanya mauaji hayo yaliyotaka kusababishwa na wivu wa kimapenzi.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo pia alimtuhumu Mabula Ntemange kuwa na mahusiano yake ya biashara alivyokuwa amejenga kijijini hapo na kuvitumia kwenye starehe na mke wake mdogo wakati yeye akiwa kwenye gereza la mahabusu la Mpanda kwa tuhuma za mauaji.
Baada ya jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kupata taarifa hizo waliweza kuchukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzima jaribio hilo kufuatia kuwa taarifa hizo kuwafikia kwa kuweza kumkamata mtuhumiwa Mbasa kabla hajatekeleza mauaji hayo.