Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kuoa mtoto wa kidato cha kwanza

Lindi Akamatwa (600 X 338) Mbaroni kwa kuoa mtoto wa kidato cha kwanza

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Hashim Komba Hashim Komba akiwa na Viongozi wengine kwenye msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule wamefanikisha kukamatwa kwa Shaibu Halid Makunda (28) baada ya kubaini amemuoa Binti mwenye umri wa miaka 17 ambaye alitakiwa aanze kidato cha Kwanza January hii na hajaripoti Shule.

DC Komba amesema Binti huyo amefaulu masomo yake vizuri na amechaguliwa kwenda Shule ya Sekondari Farm 17 iliyopo Wilayani humo lakini hajaripoti Shule kwakuwa ameolewa.

DC Komba amesema Kijana huyo amekamatwa na atapandishwa Mahakamani na Wazazi wa Mtoto huyo wanatafutwa kwa kuruhusu Mtoto wao aolewe.

“Unamuoa Mtoto wa darasa la saba ambaye alitakiwa kuwa Shule!?, sio zama hizi, jambo hili limenisikitisha sana, niwaombe Wazazi na Walezi tusiache haya yatendeke, Mtoto wa mwenzio ni wako, unapoona Mtoto ameolewa na ukakaa kimya hatuwatendei haki Watoto ni ni dhambi kwa Mungu, tuwaache Watoto wasome”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live