Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kumuua mume kwa rungu

Maasia Rungu 0 Mbaroni kwa kumuua mume kwa rungu

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limethibitisha kumshikilia Mwanamke aitwaye Aurelia Kalolo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 kwa kosa la kumpiga kichwani kwa kutumia rungu Mumewe Williad Ngamema ambaye ni Balozi wa Kitongoji cha Iwengi Kijiji cha Ukumbi Kata ya Ukumbi na kumsababishia kifo .

Ndugu pamoja na Majirani wamesema kulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara kati ya wawili hao na siku ya tukio walikuwa na ugomvi tangu asubuhi ambapo Jirani mmoja alipita nyumbani na kukuta wanagombana huku Mke akiwa ameshika rungu hivyo akawasuluhisha na Mwananke akaondoka na kwenda klabu inayouza pombe “Aliporudi nyumbani usiku ugomvi uliendelea na akampiga Mumewe kwa rungu hafi kufariki”

Mtendaji wa Kijiji hicho cha Ukumbi Mariam Kaduma amesema alipatiwa taarifa saa tisa usiku na alipofika nyumbani kwa Wanafamilia hao alikuta Mume amefariki hivyo akamshikilia Mwanamke huyo na kupiga simu Polisi ambao walifika na kumkamata na upelelezi unaendelea.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justine Lazaro Nyamoga amefika pia msibani na kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Familia ambapo amesema Balozi huyo ndiye alikiwa anategemewa na Familia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live