Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia kijana mmoja (35) mkazi wa kijiji cha Ilangali kata ya Manda tarafa ya Mpwayungu wilaya ya Chamwino kwa tuhuma za kumua baba yake mzazi (54) akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake.
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia kijana mmoja (35) mkazi wa kijiji cha Ilangali kata ya Manda tarafa ya Mpwayungu wilaya ya Chamwino kwa tuhuma za kumua baba yake mzazi (54) akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno amesema mara baada ya uchunguzi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.