Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kumchungulia mwanamke akiwa chooni na kumrekodi video

66087f07bb9a95f1 Mbaroni kwa kumchungulia mwanamke akiwa chooni na kumrekodi video

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mark Ambeyi Mutongoi ameshtakiwa katika mahakama moja jijini Nairobi kwa kumrekodi kisiri Margret Wangari akiwa chooni. Kulingana na kiongozi wa mashtaka, mlalamishi alikuwa amesimama katika Kituo cha Mafuta cha Rubis mtaani Westlands wakati aliamua kuingia msalani Ambeye alimfuata na kuweka simu yake karibu na dirisha ambapo alimrekodi lakini kitendo hicho kilinaswa na CCTV.

Mwanamume mmoja amshtakiwa katika mahakama moja jijini Nairobi kwa madai ya kumrekodi mwanamke akiwa msalani katika kituo cha mafuta.

Ripoti zinadai kuwa Mark Ambeyi Mutongoi alitumia simu yake kumrekodi kisiri Margret Wangari bila idhini yake akiwa chooni mnamo Oktoba 7, katika Kituo cha Mafuta cha Rubis mtaani Westlands.

Amrekodi msalaniKulingana na kiongozi wa mashtaka Robert Ogallo, tukio hilo lilitokea mwendo wa saa nne usiku wakati mlalamisishi alikuwa amesimama katika kituo hicho kununua mafuta kwenye barabara ya Ojiji.

"Aliamua kuingia chooni hapo ndipo mshtakiwa alitokea na simu yake na kuanza kurekodi," Ogallo alisema kama alivyonukuliwa na The Star.

Ambeyi alimfuata na kuweka simu yake karibu na dirisha ambapo alimrekodi mlalamishi.

Lakini kitendo hicho kilinaswa na kamera za CCTV bila mtuhumiwa kujua.

Wakati Wangari alifahamishwa kilichotokea, aliandikisha taarifa katika Kituo cha Polisi cha Parklands ambapo baadaye Ambeyi alikabiliwa na mashtaka.

"Alitazama kanda hiyo ya CCTV na kuthibitisha kweli ilikuwa yeye ndiye alirekodiwa," aliongezea Ogallo.

Taarifa za wafanyakazi katika kituo hicho cha mafuta pia zilichukuliwa na kutumika kama ushahidi katika kesi hiyo.

Haki ya faraghaKulingana na katiba ya mwaka 2010, sehemu ya 31 kila mtu ana haki ya faragha.

Sheria hiyo inazuia kuchukuliwa ama kunakiliwa kwa takwimu za mtu ama kusambaza habari zake za kibinafsi bila idhini yake.

Hii ni kutokana na teknolojia ya sasa ya video na picha ambazo zinaweza kusambazwa mitandaoni kuchafulia waathiriwa jina ama kuwadunisha.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke