Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kumbaka mjamzito

Mama Wajawazito Mbaroni kwa kumbaka mjamzito

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 25 ( jina limehifadhiwa) mkazi wa mtaa wa Ilazo jijini Dodoma kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa mtaa wa Kisasa

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 22,2021 jijini Dodoma kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyaanga amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 20,2021 majira ya saa kumi alfajiri huko mtaa wa kisasa kata Makulu jijini Dodoma.

Kamanda Lyanga amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa alimvamia mwanamke huyo akiwa amelala na kumfanyia kitendo hicho kilichompelekea kupata maumivu makali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live