Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kula njama kumuozesha mwanafunzi

0c20cf9ab6c6e8edaddce9211a53733c Mbaroni kwa kula njama kumuozesha mwanafunzi

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Katavi linawashikilia wakazi watatu wa wilaya ya Tanganyika wakiwemo wazazi kwa kula njama ya kumuozesha mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 16 kwa mahari ya Sh milioni moja.

Mwanafunzi huyo anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Luhele, wilaya ya Tanganyika aliozeshwa kwa kijana mwenye umri wa miaka 18.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amethibitisha kukamatwa kwa watu hao watatu akiwamo baba wa kambo wa mwanafunzi huyo, mama yake mzazi, pamoja na Balozi wa Mtaa wa Idoselo.

Kamanda Kuzaga alisema watuhumiwa hao walikamatwa Februari 7, mwaka huu saa 8:20 mchana katika kitongoji cha Luhafi kilichopo kijiji cha Vikongwe, wilayani Tanganyika.

Alisema Januari, mwaka huu watuhumiwa hao walikutana na Balozi wa Mtaa Idoseko kupanga mahari ya Sh milioni moja.

"Baada ya kikao hicho msichana aliitwa na kuelezwa mipango ya kuolewa kwake lakini hakukubaliana nayo, mama yake mzazi alimfukuza binti yake huyo nyumbani," alisema Kamanda Kuzaga.

Alisema baada ya msichana huyo kufukuzwa kwao aliamua kwenda nyumbani kwa mama mzazi wa kijana huyo na kuanza kuishi naye.

Alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Chanzo: habarileo.co.tz