Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kukutwa na sare za Polisi, JWTZ, Suma JKT

Mbaroni Kwa Kukutwa Na Sare Za Polisi, JWTZ, Suma JKT Mbaroni kwa kukutwa na sare za Polisi, JWTZ, Suma JKT

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Yohana Magota (37), mkazi wa eneo la Mafisa katika Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Suma JKT pamoja na za kampuni ya ulinzi ya Jambo Security Guard.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari mosi, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu makosa ya jinai yaliyotokea Januari mkoani hapa.

“Mtuhumiwa huyo alikutwa eneo la Mafisa, Manispaa ya Morogoro akiwa na kofia nyeusi mali ya Jeshi la Polisi, kofia ya JWTZ, sare ya Suma JKT na za kampuni ya ulinzi ya Jambo,” amesema Kamanda Mkama.

Chanzo: Mwananchi