Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Meno 2023 06 10 At 8.jpeg Mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limemkamata Adam Mgunda (29) Mkazi wa Ilula kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema katika oparesheni iliyofanyika October 01, 2023 hadi October 31 Mtuhumiwa alikutwa na vipande vitano vya meno ya tembo ambavyo alikuwa amehifadhi kwenye mfuko wa sandarusi akiwa anasafirisha kwa pikipiki.

Katika hatua nyingine ROC Bukumbi amesema Polisi Iringa kwa kushirikiana na Askari wa Uhifadhi wa Wanyamapori wamefanikiwa kukamata vipande 25 vya meno ya tembo ambavyo vilitelekezwa na Mtu/Watu ambao bado hawajafahamika vikiwa kwenye mifuko mitatu.

Katika tukio jingine Polisi wamekamata silaha moja aina ya gobore iliyotengenezwa kienyeji iliyotelekezwa katika shamba la David Magava maeneo ya Kisovelo Mkoani Iringa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live