Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kukutwa na fuvu la bimadamu

EATVSS Mbaroni kwa kukutwa na fuvu la bimadamu

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Taimu Kaogoma mkazi wa Kijiji cha Gwanupu wilayani Kakonko mkoani humo kwa Tuhuma za kukutwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu ikiwemo fuvu la kichwa na mfupa wa taya.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Kamanda wa Polisi Kigoma ACP Felomon Makungu amesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa Agosti 25 mwaka huu.

Aidha Kamanda Filemon amesema aina hiyo ya matukio imekuwa ikijirudia mkoani Kigoma kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu wanaoamini kufanikiwa kupitia imani za kishirikana na hivyo akawataka wakazi hao kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live