Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kuiba pikipiki, kumiliki gobore

MBARONI.jpeg Mbaroni kwa kuiba pikipiki, kumiliki gobore

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha kuwashikilia watu watatu ambapo wawili kati yao wanadaiwa kuhusika na wizi wa pikipiki, huku mmoja akikamatwa na bunduki aina ya gobore.

Akizungumza leo Mei 6,2024 Mkama amesema: "Watuhumiwa hao wanadaiwa kuiba pikipiki wilaya za Kilosa na Morogoro ambao ni Edson Msowela (27), mkulima na mkazi wa Mvumi huyu alikamatwa akiwa na pikipiki aina na Haoujue"

"Ally Waziri (30), mfanyabiashara na mkazi wa Dumila yeye alikamatwa na pikipiki aina ya Haojue wakati huohuo tunamshikilia, Shaban Shamte (30) yeye amekamatwa akiwa na silaha aina ya gobore na anaitumia kwenye kufanya uhalifu," amesema.

Kamanda Mkama amesema jeshi hilo limeendesha operesheni ambapo zaidi ya pikipiki 100 zilizokuwa zikijihusisha na uhalifu mkoani Morogoro zimekamatwa ambapo uchunguzi unaendelea na watakaothibitika kufanya uhalifu, watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live