Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Michael Martini (30) mkazi wa kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa tuhuma ya kuwabaka watoto watatu wenyewe umri kati ya miaka 10 na 12 wa darasa la nne na la tatu wa shule ya msingi iliyopo Bukoba.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Maketi Msangi akizungumza na waandishi wa habari Mei 26, 2022 amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ukatili huo ulifanyika Februari mwaka huu wakati watoto hao walipokuwa wameenda kuchanja kuni katika msitu wa Serikali wa Rwendimi uliopo kata ya Ijuganyondo Manispaa ya Bukoba.
Msangi amesema siku ya tukio mtuhumiwa aliwavizia akawakamata na kuwatishia kuwakata kwa panga kama watapiga kelele na kisha kuwabaka.