Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa Kumiliki Karakana ya Silaha

Onesmo Lyanga?fit=876%2C657&ssl=1 Mbaroni kwa Kumiliki Karakana ya Silaha

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumiliki karakana ya kutengeneza silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali na kuziuza kwa wahalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga, amesema kufuatia msako uliofanyika katika Kijiji cha Chilendu, Kata na Tarafa ya Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa walikamatwa watuhumiwa hao, ambao majina hayakutajwa, wakimiliki karakana ya kutengenezea silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali.

Lyanga amesema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na gobole tano zilizo tayari, baruti gramu 408, goroli vipande vya chuma 40, fremu za silaha mbili na vifaa mbalimbali vya uchongaji wa silaha hizo.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz