Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa Kujiibia na Kuripoti Polisi

Pingu 4 Mbaroni kwa Kujiibia na Kuripoti Polisi

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linshikiria Maila Majula (29) mkazi wa Makongo juu kwa madai ya kutoa taarifa za uongo kituo cha Polisi Msimbazi za kuibiwa gari lake aina ya Toyota IST rangi ya bluu.

Uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa alipewa milioni kumi na kaka yake ili akaziweke benki matokeo yake akazitumia kwa matumizi yake binafsi na kuamua kutengeneza tukio la kufikikirika kuwa pesa ile na gari viliibwa wakati yeye aliposhuka kwa muda na aliporudi hakukuta gari iliyokuwa na pesa .

Baada ya kumtilia mashaka mtoa taarifa ilibainika kuwa taarifa hizo ni za uongo, na ilibainika gari hilo alikuwa amelificha maeneo ya Tabata kwa Swai ambako lilipatikana kabla ya kwenda kituoni kutoa taarifa za kuibiwa kwa gari hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live