Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa Kujifanya Polisi kwa Miaka Saba

Mahakama Pc Data Mbaroni kwa Kujifanya Polisi kwa Miaka Saba

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Nyamanoro Mkoa wa Mwanza, Abdul Hamad Nassoro (49) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa Polisi kwa zaidi ya miaka saba.

Mkazi huyo amefikishwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo wilayani Igunga, Juhudi Mgonya akikabiliwa na mashtaka mawili.

Akimsomea mashitaka mawili mbele ye hakimu wa mahakama ya mwanzo Juhudi Mdonya, mwendesha mashitaka wa polisi wilaya ya Igunga, Ellymajid Kweyamba ameiambia mahakama kuwa katika shitaka la kwanza linalomkabili mshitakiwa huyo kuwa Desemba 24, 2021 mchana katika maeneo ya kituo cha polisi kata ya Igunga mjini, mshitakiwa alikamatwa na vitambulisho mbalimbali vya kazi huku akijitambulisha kuwa yeye ni mwajiriwa wa Jeshi la polisi Tanzania.

Mwendesha mashitaka amesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 100(b) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2016.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na amepelekwa mahabusu baada ya kukosa mdhamini.

Mwendesha mashtaka aliendelea kuiambia mahakama kuwa kosa la pili linalomkabili mshitakiwa Nassoro ni wizi wa kuaminiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live